Msanii
wa muziki Linah Sanga amefunguka na kuzungumza hukusu ujauzito wake
baaada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kulizungumzia suala hilo.
Akiongea na Bongo5 wiki hii akiwa pamoja na mpenzi wake huyo ambaye pia
ni bosi wake, Linah alidai anafuraha kuwa mjamzito kwa kuwa ni kitu
ambacho alikuwa nakitamani kwa muda mrefu.
“Ninafuraha kubwa kwa sababu ni kitu ambacho kama mwanamke nilikuwa
nakitamani siku zote kwamba na mimi nije niitwe mama, nafuraha nimepata
mtu sahihi wa kuzaa naye na kuamua kulea naye watoto,”alisema Linah huku
akiwa mwenye furaha.
Kwa upande wa mpenzi wake ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni Drops Up
Entertainment ambayo inamsimamia Linah, alisema wao kama kampuni
wamejipanga kuhakikisha Linah wanamsfikisha mbali zaidi.
“Tuna mipango mikubwa kwa Linah kwa sababu kila kitu ambacho tulikuwa
tunafanya kwa mpango tuliangalia sasa hivi yupo kwenye hali fulani, kwa
hiyo management imejipanga kuhakikisha Linah anafika sehemu fulani. Pia
kwa mwaka huu Linah time table yake imetimia, ana audio zakutosha pamoja
na video za mwaka mzima,”

0 comments:
Post a Comment