HUYU NDIYE ANAYEDAIWA KUMUUZIA CHETI CHA KIDATO CHA NNE RC MAKONDA.
Mwandishi anayedaiwa kumpa cheti cha kidato cha nne Makonda, ambaye anajitambulisha kwa jina la Paul Christian.
“Paul Makonda nimemfahamu kupitia habari, na jina wanavyolitaja (waliotunga taarifa ya mtandaoni) wanakosea kwani mimi naitwa Paul Pierre Christian Kagezi, hatuna uhusiano, mimi Mhaya yeye Msukuma.” Alisema watu wanaooanisha majina pasipo kufanya utafiti wa kutosha, wangeuliza kwanza kabla ya kutoa na kusambaza taarifa kwenye mitandao.
“Taarifa hizo (za kumpa cheti Makonda) si za kweli kwa sababu huwezi kutoa cheti wakati umepata daraja la kwanza kidato cha sita, utakwenda vipi chuo kikuu? Sasa niliwezaje mimi kwenda chuo kikuu halafu kwa wakati huo nimpe naye aende chuo kikuu?”Alihoji.
Cristian aliendelea kudai kuwa katika kidato cha tano na sita, alichukua mchepuo wa sayansi masomo ya Fizikia, Kemia na Hesabu (PCM), hivyo si rahisi kutoa cheti hicho kwani angeshindwa kumudu huko alikokwenda.
Alihoji kama Makonda hakufanya vema kidato cha nne au hakusoma kidato cha sita, akatumia cheti cha mtu mwingine, angeweza vipi kufanya vema katika mitihani yake ya chuo kikuu?
Alifafanua kuwa watu wamekuwa wakipika na kuoanisha majina yao, huku akiendelea kukanusha kuhusu taarifa hizo.
“Kama wanataka kumpata huyo bwanamdogo (Makonda) kwa njia hiyo wamemkosa, kwani kwa mantiki nimekuuliza ukipata daraja la kwanza kidato cha sita lazima uende chuo kikuu?” Alihoji baada ya kushindwa kujibu swali la mwandishi kuhusu chuo kikuu alichosoma na ilikuwaje akawa mwandishi wa habari.
Christian aliendelea kudai kuwa kutumia cheti kimoja kwa vyuo viwili vya Serikali, ni jambo lisilowezekana akimaanisha Makonda asingeweza kutumia cheti alichokuwa akitumia yeye.
“Sera ya Serikali ni kwamba unapata asilimia 100 ya mkopo, inakuwaje mtu huyo nimpe cheti changu wakati huo naye anakwenda chuo kikuu ambacho nacho ni cha Serikali?” Aliendelea kuhoji.
“Huyo bwana anajitegemea yeye kama yeye, na walichokifanya wao (waliosambaza taarifa mtandaoni) kwa makusudi yao bila shaka wana lengo lao, wao wametaka kuingiza hoja ambazo hazina mashiko. “Cheti cha daraja la kwanza unauza kwa gharama gani? Nimesoma shule ya msingi na sekondari, (Makonda) alikuwa na fedha kiasi gani za kunipa ili nimuachie cheti? Inaweza kukuingia akilini kweli?”Alihoji Christian.

0 comments:
Post a Comment