Wednesday, February 22, 2017

Weekend iliyopita tulipata nafasi ya kumsikia msanii mpya ambaye amesainiwa katika lebo ya muziki ya mwanadada Vanessa Mdee inayofahamika kama Mdee Music na kupata nafasi ya kuzindua video yake mpya pande za CLub Next Door.

Msanii ambaye anafahamika kwa jina la Mimi Mars, na taarifa zinasema kuwa ni ndugu wa damu kabisa na msanii Vanessa Mdee.
Wapo wengi ambao walidhani kwamba ilikuwa ni rahisi tu kwa Mimi Mars kujiunga na Mdee Music,ila yeye ametusanua ni ugumu gani ambao amepitia mpaka kusainiwa katika lebo hiyo ya dada yake.
“Nimepitia vitu vingi sana mpaka yeye kukubali kunisaini, kwasababu nilikuwa nataka kuanza muziki kitambo kama miaka mitatu iliyopita hivi, lakini alikuwa ananiambia bado sijawa tayari kwenye mambo kama sauti na vitu kama hivyo. Kwahiyo nilikuwa na pitia mitihani mingi mpaka yeye amekuja kukubali ni baada ya kusikia single yangu ya kwanza ndipo akasema YES.” Alisema Mimi Mars.

0 comments:

Post a Comment