Tuesday, February 14, 2017

Kell Brook

Mwanamasumbwi Kell Brook anataraji kutetea mkanda wake wa ubingwa wa dunia IBF uzito wa walter dhidi ya bondia Errol Spence Jr kutoka nchini Marekani.


Pambano hilo linataraji kufanyika Sheffield tarehe 20 May, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waandaaji wa pambano hilo kupitia katika akaunti ya Twitter.

Brook, 30, hajapanda ulingoni kwa kipindi kirefu sasa toka alipopokea kichapo kikali katika pambano lake la mwisho dhidi ya Gennady Golovkin lililofanyika mwezi September mwaka jana.
Errol Spence

 
Mara baada ya kupoteza katika pambano hilo Brook alilazimika kufanyiwa upasuaji mdogo sehemu za jicho ni mara baada ya kuchanika kufuatia konde zito alilopigwa na bondia Kazakh.

Brook alipata mkanda wa IBF mara baada ya kumchapa vikali Shawn Porter mwezi August 2014 na baadae akautetea mkanda wake dhidi ya mabondia Jo Jo Dan, Frankie Gavin na Kevin Bizier.

Kwa upande wa Bondia Spence ambae ndie mpinzani wa Brook mwezi may hadi sasa ameshazipiga katika mapambano 21 ya kimataifa na kufanikiwa kushinda kwa KO katika mapambano 18.

0 comments:

Post a Comment