![]() |
| Msemaji wa klabu ya Azm FC Japha Iddy Maganga (kulia) akiwa na Meneja wa klabu ya Red Arrows ya Zambia Meja Bruce Milunga (kushoto) |
Klabu ya soka ya Azam inataraji kukipiga katika mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya Red Arrows ya Zambia katika mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi.
Akizungumzia mchezo msemaji wa klabu ya Azam Japha Iddy Maganga amesema klabu ya Azam itautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi kuelekea katika mchezo wao wa kombe la Shirikisho unaotaraji kupigwa mwezi March.
Japha amesema Azam itapata mazoezi tosha katika mchezo huo kwani timu zinazomilikiwa na majeshi ni timu ambazo zimekuwa na ushindani mkubwa katika mchezo wa soka.
Kwa upande wa Meneja wa klabu ya Red Arrows Meja Bruce Milunga amesema kikosi chake kimekuja nchini kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka nchini Zambia.
Meja Bruce amesema hapo awali walikuwa wakipige dhidi ya klabu ya Simba lakini hilo lilishindikana ndipo busara ilipotumika na kufanikiwa kupata mchezo wa kirafiki dhidi ya Azam Fc.
Katika hatua nyingine Meja Bruce amesifu miundombinu iliyopo katika uwanja wa Azam Complex kuwa ni miundombinu ya kisasa na yenye viwango vya kimataifa.


0 comments:
Post a Comment