Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda,
ametangaza kuunda serikali sambamba na utawala uliopo Rwanda, lakini
itakayokuwa ikifanya kazi nje ya nchi.
Thomas Nahimana ambaye ni kasisi wa zamani anayeishi nchini Ufaransa ametangaza kuunda serikali hiyo itakayofanyia kazi uhamishoni.
Katika mazungumzo na BBC, mwanasiasa huyo anasema lengo la serikali yake ni kuiondoa madarakani serikali ya rais Paul Kagame, anayemlaumu kuvunja sheria na kukandamiza wananchi.
Bw Nahimana, ambaye ni mhutu, amelaumiwa kwa kuandika taarifa kadhaa za kikabila na kumkosoa rais Paul Kagame.
Chama chake cha Ishema, bado hakijaandikishwa nchini Rwanda.
0 comments:
Post a Comment