
Baada ya kuficha uhusiano wao, Mwimbaji
wa Gospo Bongo, Emmanuel Mbasha na Mshiriki wa Miss Tanzania 2008,
Jacqueline Chuwa, sasa siyo siri tena kwani Wikienda lina picha zao
mubashara wakiwa kwenye mahaba niue. Mtu aliyevujisha picha hizo,
aliliambia Wikienda kuwa, Mbasha na Jack kwa sasa hawajifichi tena kwani
wamekuwa wakionekana sehemu mbalimbali kama kanisani, sehemu za starehe
na hivi karibuni walikuwa wakijiachia Siku ya Wapendanao huku wakiwa
kwenye mavazi rasmi ya wapenzi.
“Naona wameamua kuweka mambo mubashara
kabisa kwa sababu Mbasha ameshasarenda kwa aliyekuwa mkewe, Flora Mbasha
maana sasa ni malavu kwa kwenda mbele. Ukikutana nao hata hawajifichi
baada ya Wikienda kuwaweka hewani,”
kilimwaga ubuyu chanzo chetu. Baada ya
kupata ubuyu na picha hizo kutoka kwa sosi, mwanahabari wetu alimwendea
hewani Jack ambaye muandaaji wa Shindano la Miss Tanzania mkoani
Kilimanjaro ambapo alifunguka kuwa, hapendi kuzungumzia kiundani mambo
yake ya uhusiano lakini anachojua ni kwamba, yeye na Mbasha ni marafiki
na muda ukifika, kama kuna kinachoendelea ataweka wazi kila kitu. “Muda
ukifika nitaweka wazi kila kitu kama kuna mambo ya ndoa na uchumba, wala
msiwe na wasiwasi ninyi mtaona tu, suala hilo huwa halina kificho,”
alisema Jack kwa bashasha.
Alipotafutwa Mbasha simu yake iliita
bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu pamoja na
kwamba ulionesha kupokelewa. Wiki mbili zilizopita, Wikienda ndilo
lilikuwa la kwanza kuripoti juu ya uhusiano wa Mbasha na Jack huku
wawili hao wakija juu lakini sasa mapenzi yao siyo siri tena.
0 comments:
Post a Comment