Ligi Kuu Soka Tanzania bara inataraji
kuendelea tena siku ya Jumatano kwa michezo kadha kupigwa.
Mabingwa watetezi wa ligi hiyo,
Young Africans watakuwa wenyeji wa klabu ya Ruvu Shooting katika mchezo utakaofanyika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Michezo mingine inataraji kupigwa
mwishoni mwa juma ambapo, Simba SC itakipiga dhidi ya Mbeya City katika Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Toto Africans itakipiga dhidi ya
mbao Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza huku Kagera Sugar
ikiikaribisha Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Azam FC pia itacheza dhidi ya
Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Chamazi.
Katika hatua nyingine Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limerejesha tena mechi za Ligi Kuu kwenye
Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na Jumapili Machi 5, mwaka huu Mtibwa Sugar
itaialika Young Africans kwenye uwanja huo katika mfululizo wa mechi za Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya
Vodacom utachezwa katika Uwanja wa Uhuru ambapo African Lyon itaialika Mwadui
ya Shinyanga wakati Ndanda FC itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja
wa Nangwanda Sijaona.

0 comments:
Post a Comment