Kauli ya meneja huyo imekuja mara baada ya Ibrahimovic, 35, kuiwezesha
United kutwaa taji la EFL kwa kuifungia mabao mawili ya muhimu katika ushindi
wa mabao 3-2.
Katika mchezo huo wa fainali ulioikutanisha United dhidi ya Southampton
katika dimba la Wembley, Zlatan alienda kambani dakika ya 19 na dakika ya 87.
Mourinho amesema hana kawaida ya kumbembeleza mchezaji, hana kawaida ya
kumbembeleza mchezaji aongeze mkataba badala yake mashabiki ndio wanatakiwa
kumshawishi mchezaji abaki katika klabu lakini inapokuja juu ya sakata la Ibrahimovic
ni vema akabaki.
Wakati huo huo Mourinho, aliwahi kuwa Kocha wa Ibrahimovic wakati
akiinoa klabu ya Inter Milan, lakini baadae akaihama klabu hiyo na kuelekea
nchini Hispania kukipiga katika klabu ya Barcelona mwaka 2009.
Mourinho amesema wakati Ibrahimovic alipokwenda Hipania alijisikia
vibaya sana, lakini alipamua kukipiga katika klabu ya Manchester United ni
jambo ambalo lilimfurahisha sana.


0 comments:
Post a Comment