Monday, February 13, 2017



Mwanamasumbwi nguli duniani Manny Pacquiao amewataka mashabiki wake kumchagulia bobdia wa kupambana nae katika kutetea taji lake la WBO uzito wa walter.


Kupitia katika akanti yake ya twitter Pacquiao ameorodhesha orodha ya majina ya mabondia anaotaka kuzichapa nao, huku akiwataka wapenzi wake katika mchezo wa masumbwi wapige kura ili kumchagulia bonda mmoja atakaepa nae ulingoni mwezi November.


Mabondia hao ni Amir Khan, Kell Brook, kutoka Uingereza, Jeff Horn kutoka Australia na Terence Crawford kutoka Marekani.

Pacquiao amesema pambano hilo litafanyika katika falme za kiarabu.

0 comments:

Post a Comment