Tuesday, February 14, 2017

Ikiwa suala la lebo linaendelea ku-take over katika industry ya music hapa Bongo ni mengi ambayo tunaendelea kuyashuhudia kila kukicha.

Na baadhi kati ya hayo ni kuwashuhudia wakali ambao walifanya vizuri kwa kiasi chao kipindi cha nyuma ambapo walikuwa wakifanya music kama single artist na baadaye kuamua kusainiwa na lebo fulani na maisha yakaendelea.
Mfano wa hao ni kama Rich mavoko ambaye sasa hivi yuko chini ya WCB Wasafi, Big Jahman ambaye kasainiwa na Fid Q kwenye lebo ya Cheusi Dawa na wengine kibao.
Sasa Perfect255 imepiga story na hitmaker wa ngoma ya Phone Benpol na kutaka kujua endapo atahitaji kusainiwa kwa hapa Bongo ni lebo ya msanii gani itamfaa.
“Kwa hapa Bongo labda Fid Q akiwa na lebo naweza kufanya naye kazi, kwasababu ni mtu ambaye ameshafanya vitu vingi bila faida nikiwa namaanisha kuwa amesha saidia wengi bila kupata faida. Mtu wa hivyo ukifanya naye kazi pesa inakuwa sio kila kitu kwake. Hamuwezi kugombana.” Alisema Benpol.
Bonyeza play kwenye video hii hapa chini kumsikiliza Benpol akifunguka juu ya mchongo huo.

0 comments:

Post a Comment