Mwenyekiti wa chama cha soka nchini Uingereza Greg
Clarke ameweka wazi mpango wake wa kujiuzulu kama serikali ya Uingereza
haitamuunga mkono katika jitihada zake za kuunda upya chama cha soka nchini
humo.
Clarke aliweka wazi mpango wake wa kujiuzulu usiku wa
jana na sasa atasubiri mjadala unaotaraji kufanyika siku ya Alhamisi katika
bunge la Uingereza.
Mjadala huo umeandaliwa na Mbnge Damian Collins ambae
pia ni Mwenyekiti wa utamaduni, Habari na Michezo nchini Uingereza.
Katika barua yake ya kujiuzulu, Clarke amesema mchezo
wa soka nchini Uingereza unahitaji mabadiliko ya hali ya juu lakini amekataa
kukiri kwamba Chama cha soka FA kinadhorotesha mchezo wa soka nchini humo.
Clarke amesema sasa inabidi mambo ya soka yaendeshwe
kwa uwazi zaidi hususan katika maamuzi ya mambo mbalimbali ili kufanya mchezo
wa soka uzidi kusonga mbele.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa FA alietangaza nia yake
ya kujizulu amesema anafahamu kwamba mabadiliko hayawezi kupatikana kwa urahisi
lakini anaamini yatapatikana.

0 comments:
Post a Comment