Rapper mkongwe kutoka A Town, Joh Makini akiwa anawakilisha Weusi, na hivi sasa anafanya vyema na ngoma yake ‘Waya’ amefunguka juu ya ngoma ya Fid Q ‘Kemosabe’.
Joh Makini adai ngoma mpya ya Fid Q ‘Kemosabe’ ni ngoma kali sana na yeye amependa jinsi ambavyo Fid Q amebadilika katika flow kwani imekuwa tofauti na kazi zake nyingi za nyuma.
Ngoma kali sana, nimependa jinsi ambavyo Fid Q amebadilika katika flow kwani kazi hiyo imekuwa tofauti na kazi zake nyingi alizofanya kipindi cha nyuma”. alisema Joh Makini kwenye FNL.
Mbali na hilo, Katika hatua ambayo pengine haikutegemewa na wengi kutokana na tetesi kuwa kuna bifu kati ya Mwamba wa Kaskazini na Fid Q. kuthibitisha jambo hilo rapper kutoka Rock City (Mwanza), aliamua kuwaonesha watu kwamba hakuna bifu kati yao.
Kupitia mtandao wa Instagram, Fid alipost kipande cha video mpya ya Joh Makini na kuandika, “#newvideoalert WAYA toka kwa MWAMBA WA KASKAZINI @johmakinitz ( link ipo kwenye BIO yake… nenda kajionee MAUNYAMA.”

0 comments:
Post a Comment