Shirikisho
la soka nchini TFF lipo katika mazungumzo na makampuni ya mitandao ya
mawasilino nchini ili kufanikisha mpango wa kuchangisha fedha kwa ajili ya
maandalizi ya timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti
Boys).
Afisa habari
wa TFF Alfred Lucas amesema mpaka sasa mazungumzo hayo yamefikia pazuri na
wanaamini mambo yatakapokaa swa kila mtanzania atakuwa na uwezo wa kuchangia
fedha kwa ajili ya kuiwezesha timu hiyo ili ifanikishe azma ya kwenda nchini
Gabon kupambana vilivyo.
Wakati huo
huo ligi kuu ya soka ya wanawake Tanzania Bara hatua ya Sita bora imeanza rasmi
jana katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, huku shirikisho al soka
nchini TFF likikiri kufurahishwa na mwanzo wa hatua hiyo.
Afisa habari
wa shirikisho hilo Alfred Lucas amesema baada ya matokeo ya jana ya mchezo wa
ufunguzi, wanaamini timu nyingine shiriki katika hatu aya sita bora zimejipanga
vilivyo kwa ajili ya kuuwani ubingwa wa Tanzania bara.

0 comments:
Post a Comment