Uongozi wa
klabu ya Simba umetoa shukurani kwa mashabiki na wanachama wao kwa ustaarabu
waliouonyesha wakati wa mchezo wao dhidi ya Young Africans ambao ulimalizika
kwa kupata ushindi wa mabao mawili kwa moja.
Shukurani
kwa mashabiki na wanachama wa Simba zimetolewa na mkuu wa idara ya habari na
mawasiliono Haji Manara alipozungumza na vyombo vya habari mchana wa leo kwenye
ukumbi wa kamao makuu ya klabu hiyo yaliopo Mtaa wa Msimbazi Dar es salaam.
Haji amesema
mashabiki na wanachama wa Simba walionyesha ustaarabu wa hali ya juu kutokana
na maamuzi yaliyochukuliwa dhidi ya kikosi chao ambayo yalikua halali tangu
dakika ya kwanza hadi mwisho.
Hata hivyo
Haji Manara ametoa wito kwa mashabiki na wanachama wa Simba kuendelea kuwa kitu
kimoa katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa msimu huu, na pia amewataka
kufika viwanjani bila kusita kuishangilia timu yao ili iweze kuhitimisha azma
ya kutwaa ubingwa kwa kushinda michezo saba ya ligi iliyobaki.
Wakati huo
huo Manara ametoa shukurani kwa Serikali, taasisi na watu mbali mbali ambao
walihakikisha mchezo wa jumamosi unachezwa kwa amani na utulivu.

0 comments:
Post a Comment