Thursday, March 16, 2017



Roger Federer amepata ushindi mbele ya Rafael Nadal katika mchezo wa tennis na sasa amefanikiwa kutinga katika hatua ya nane bora katika michuano ya wazi ya Indian Wells.


Katika mchezo huo Federer raia wa Uswis alipata ushindi wa seti 6-2 6-3.

Huu ni ushindi wa tatu mfululizo kwa Federer hii ikiwa ni mara ya 36 kwa wawili hao kukutana, toka walipokutana kwa mara ya kwanza katika jiji la Miami miaka 13 iliyopita.


Nadal, 30, alikuwa akimsumbua sana Federer kwa miaka kadhaa katika michuano mbalimbali lakini kwa sasa kibao kimegeuka na amemshinda katika michuano kadhaa ikiwemo michuano ya wazi ya Australia.


Mara baada ya kupata ushindi huo Federer amesema amefanya vema katika mchezo huo na anashukuru kwamba amefanikiwa kutinga katika hatua inayofata.

Sasa atakutana na Nick Kyrgios, toka Australia ambae yeye amefanikiwa kumfedhehesha Novak Djokovic kwa kumshinda kwa seti 6-4 7-6 (7-3).

Kyrgios, 21, ameonesha kiwango kizuri katika mchezo huo kiwango ambacho kimempelekea kupata matokeo hayo.


Kinda huyo amezizima ndoto za Djokovic ambae alikuwa anatafuta ushindi ili aweze kusonga katika hatua inayofata na kutafuta taji katika michuano hiyo inayoendelea lakini kupoteza kwa seti mbili mfululizo na kuwa amefungwa Kyrgios 2-0 kwani alipoteza pia katika mchezo mwingine uliopigwa huko Acapulco siku 12 zilizopita.



Mara baada ya kupata ushindi huo Kyrgios amesma alikuw a akianzisha vema mipira na hivyo kutengeneza hofu kwa mpinzani wake. Amesema ushindi huo umemjenga kisaikolojia na atajitahidi kumshinda kila anaekutana nae mbele yake.


Kyrgios anashika nafasi ya 15 kwa ubora duniani.


Wakati huo huo Mjapan Kei Nishikori amefanikiwa kupata matokeo alipocheza dhidi ya Mmarekani Donald Young na kumfunga kwa seti 6-2 6-4, huku katika michezo mingine Pablo Carreno Busta pamoja na Pablo Cuevas wakifanikiwa kusonga mbele.

Mmarekani Jack Sock anaeshikilia nafasi ya 17 kwa ubora amemshinda Malek Jaziri toka Tunisia kwa seti 4-6 7-6 (7-1) 7-5.


Kwa upande wa wachezaji wawili Jamie Murray pamoja na Mbrazil Bruno Soares wamefanikiwa kusonga katika hatua inayofata mara baada ya kupata ushindi wa seti 7-6 (7-5) 6-4 dhidi ya Jean-Julien Rojer na Horia Tecau.

0 comments:

Post a Comment