Thursday, March 16, 2017


Hatimae Shirika la ndege la Malawi, Malawi Airlines, limekamilisha ahadi yake ya kufanya safari ambayo iliongozwa na wanawake pekee kuanzia marubani hadi wahudumu wa ndani ya ndege.


Ndege hiyo ilianza safari yake katika mji wa Blantyre na baadae ilitua kwa muda katika uwanja wa ndege Lilongwe na baadae ilitua Dar es Salaam.

Shirika hilo la ndege, limesema lengo la kuwatumia marubani pamoja na wahudumu wa kike pekee ni kuonyesha kwamba hata wanawake wanaweza kutekeleza mambo katika jamii.


0 comments:

Post a Comment