Thursday, March 16, 2017



Meneja wa klabu ya manchester United Jose Mourinho amemkingia kifua mkiungo wa klabu hiyo Paul Pogba kwa kusema kwamba wote wanaokikosoa kiwango kinachooneshwa na mwanandinga huyo wana wivu.

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku kadhaa zimepita toka United ilipopoteza katika mchezo dhidi ya Chelsea katika kombe la FA.

Mara baada ya kukamilika kwa mchezo huo, wadau wengi wa soka walibeza kiwango cha Pogba kwani alizidiwa kwa mbinu na Kiungo wa klabu ya Chelsea NG'olo Kante ambae hajanunuliwa kwa dau kubwa kama la Pogba.

 NG'olo Kante alinunuliwa kwa dau la paundi 32 milioni, wakati Pogba alinunuliwa kwa dau la zaidi ya Paundi 89.
 
"Nahisi kwamba ulimwengu unapoteza thamani yake, nahofia kiwango cha wivu unaoingia. Si makosa ya Paul kwamba anapokea pesa mara kumi zaidi ya wachezaji wengine waliokuwa hapo awali" Amesema Mourinho.
'

0 comments:

Post a Comment