Kuelekea
katika uchaguzi wa kumchagua rais wa shirikisho la soka barani Afrika Kamati ya
utendaji ya shirikisho hilo imefikia maazimio mbali mbali kuhusu michuano
mbalimbali ijayo.
Katika
mkutano huokuelekea katika michuano ya CHAN ya mwaka 2018 itakayofanyika nchini
Kenya Serikali ya Taifa hilo imeonekana kujitoa katika kuhakikisha miundombinu
kwaajili ya michuano hiyo inapatikana.
Ukaguzi
maalum ulifanyika chini ya Makamu wa Rais wa kwanza wa CAF Suketu Patel kati ya
February 20 hadi 24, kwa kutembelea viwanja mbalimbali vilivyopo Nairobi, Eldoret,
Meru pamoja na Machakos.
Kuhusu
fainali za 2017 za AFCON U-17 zinazotaraji kufanyika nchini Gabon. Ombi la viwanja
vya Franceville na Port-Gentil limepitisha na sasa viwanja hivyo ndio
vitakavyotumika katika fainali hizo zinazotaraji kupigwa kati ya 14 hadi 28 May
2017.
Kuhuus
fainali za AFCON U-20 Zambia kamati ya CAF imeitumia Zambia barua kuipongeza
serikali pamoja na mamlaka zinazohusika na mchezo wa soka nchini humo kikiwemo
Chama cha Mchezo wa soka Zambia FAZ kutokana na maandalizi mazuri walioyafanya.
Katika
soka la wanawake ratiba imeshapangwa kwaajili ya mashindano ya 11 ya fainali za
wanawake AFCON. Fainali hizo zitafanyika nchini Ghana 2018, kati ya Novemaba 17
hadi December 1 ya mwaka 2018.
Kwa
upande wa mtoano pamoja na kuwania nafasi ya kutinga katika fainali hizo za
wanawake itakuwa ni kati ya February 26, 2018.
Kalenda
kwa soka la wanawake nayo pia imeshaandaliwa kwaajili ya fainali za wanandinga
wenye umri cchini ya miaka 20 pamoja na 17.
Katika
hatua nyingine kamati hiyo iliiruhusu sekretariet ya CAF kuanza mchakato wa
kuitafuta nchi itakayoandaa fainali za Mataifa ya Afrika kwa wanwake ya mwaka
2020.
Maazimio
mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na kamati ya maadili kuiuhusu kamati ya
nidhamu ya CAF kujadili kesi mbalimbali ikiwemo kesi ya Rais wa COSAFA, ambae
pia ni raisi wa Shirikisho la mchezo wa soka Zimbabwe Philip Chiyangwa ambae
ameonekana kuishambulia CAF pamoja na kumshambulia Rais Issa Hayatou.
0 comments:
Post a Comment