Wednesday, March 15, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda akiwazungumza machache na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Simon Sirro.
Mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda anatimiza mwaka mmoja tangu ateuliwe kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam hivyo amekutana na wadau mbalimbali wa mkoa huo kwa ajili ya kutathmini mambo mbalimbali kwenye uongozi wake na amezungumza mambo mbalimbali ikiwemo vita ya dawa za kulevya. Namshukuru Rais Magufuli kwa kusikiliza kauli ya Mungu na kunikabidhi mamlaka ktk mkoa huu wa Dar.Navishukuru sana Vyombo vya Habari kwa kuwa daraja kati ya Serikali ya Mkoa na wananchi. Wamefanya kazi kubwa!Nawashukuru sana vijana tuliowakamata wa mwanzo(TID na wenzake), wamekuwa mfano mzuri kwa wenzao na Mungu awasaidieMwaka wangu wa II nikiwa kama RC wa Dar, kasi itaongezeka maana nimekomaa sasa. Nitahakikisha jiji linarudi kwny mstari.Kuna makampuni ya barabara mawili nimeshayapiga marufuku kwa sababu ya kujenga barabara chini ya viwango.
Katika vitu nimeweka msingi mzuri ni kinondoni, kesi za ardhi zinasikilizwa mpaka jumamosiKazi hii nimepewa na Mungu, acha idadi ya wanaomchukia Makonda waongezeka lakini niwe na uhakika na Mungu wanguTumeamua kufanya vitu hadharani kwa sababu hatutaki kupokea rushwa wala fedha haramuHatuna kisasi na mtu, ndio maana upande huo wanapigana sisi tunachekaKupitia fedha za dawa za kulevya, watu wamejenga maghorofa yanakwenda kwa kasi sana na wamefanya hata thamani ya viwanja ipande
Fedha hizi za dawa za kulevya zinaenda kukauka DSM ili kila mtu ale kwa jasho lakeTutaanza mfumo wa kutumia kadi ili tukusanye kodi yetu na kila mtu ale kwa jasho lake, kuna watu wanaficha fedhaKipindi hiki ni cha kazi. Nawapongeza wote wanaofanya kazi kwa bidii na kuifanya Serikali isimame kideteChangamoto mojawapo niliyokutana nayo ni MUDA! Muda hautoshi, nahitaji hata miaka kadhaa ili kumsikiliza kila mwananchiChangamoto nyingine ni mazoea ya Watendaji wa Serikali ktk kutoa huduma. "Njoo kesho" imekuwa kero kwangu na kwa wananchi

Kuzungushwa kwa wananchi kunapelekea changamoto katika za Serikali za Mitaa kuletwa ofisini kwangu. Hili nalo ni tatizo!

Nampongeza sana Kamishna Sirro na Awadhi (wa Usalama barabarani) kwa kusimamia ulinzi na usalama jijini Dar

Milio ya risasi ilikuwa kawaida Dar, watu waliogopa hata kwenda Mlimani City kwa hofu ya kuporwa. Tumeyakomesha yote hayo

Kuna kampuni mbili za ujenzi wa barabara nimezipiga marufuku mkoani kwangu(Dar) kwa kujenga barabara zenye viwango duni

Nilihakikisha Mahakama ya Ardhi ya Kinondoni inatenda haki na kutoa hukumu kwa wakati. Sasa wanafanya kazi hadi Jumamosi


TID akiongea ameihasa jamii athari mbali za madawa ya kulevya na kusititiza watu wawaombee waathirika waache matumizi ya madawa ya kulevya. Anasema mtumiaji anapoteza uelekeo.anasema hakuna chama kitakachoruhusu mtumiaji wa madawa ya kulevya kujiunga na chama iwapo kitakua makini( anamponda wema)


Sirro: Langu ni moja tu, kazi hii ni kubwa. Watu waendelee kutoa taarifa. Nina jambo moja tu kwa viongozi. Mkoa wa Pwani viongozi wengi wanauawa. Tuna changamoto Tanga na hata Mwanza.Kuna mazoezi ya Judo na Kareti kwenye makanisa, kwenye misikiti, kwenye nyumba za ibada kwa ujumla, tutunze sana waumini wetu. Sisi tuna mipaka lakini huwa tunatuma vijana wetu, tunawaweka watoto kwenye mazingira mabovu, Asnteni kwa kunisikiliza.


Daktari anayehusika na madawa anaongea kwa kuelezea magonjwa yatokanayo na madawa ya kulevya. Halafu inaoneka mateja wengi wapo kwenye kikao. Daktari anasema mtu akiwa anatumia madawa ni vyepesi kupata maambukizi ya UKIMWI, ULAIBU, TB, MENO. Uharibifu wa mazingira kubaka uhalifu na hivyo kuliongezea taifa gharama za kuwahudumia


Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar: Sasa RC Makonda umekomaa, haiwezekani kila anayekuchokoza ukamjibu.Tuwatazame mateja kama ndugu zetu, tusiwaue wala kuwachoma moto wafanyapo uhalifu bali tuwape msaada wanaoutaka
















0 comments:

Post a Comment