Friday, March 17, 2017


Rais mpya wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF Ahmad Ahmad amesema kazi yake ya kwanza atakayoifanya ni kukagua hesabu za fedha na kuliunda upya Shirikisho hilo mara baada ya kufanya tathmini.


Kauli ya Ahmad imekuja ikiwa imepita siku moja tu, toka alipomuangusha Issa Hayatou ambae alihudumu katika shirikisho hilo kwa miaka 29.
Katika uchaguzi uliofanyika siku ya jana, Ahmad alipata jumla ya kura 34 huku Hayatou akipata kura 20 tu.

"Nitakwenda katika makao makuu ya CAF nitaangalia yale yaliyomo ndani ya Shirikisho hilo na baada ya hapo nitafanya mabadiliko ya kiuongozi pamoja na ukaguzi wa fedha". Amesema Ahmad.

Ahmad amesema mara baada ya kuendesha zoezi hilo atafanya mkutano na waandishi wa habari ili kuwaeleza yale atakayoyabaini.

0 comments:

Post a Comment