Friday, March 17, 2017


 Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limewataka wakazi wa jiji hilo wanaoishi maeneo ya mabondeni kuondoka mara moja.

Akizungumza na wanahabari , Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Siro, amesema jeshi la polisi limejipanga vya kutosha na kusisitiza kwamba wale wote watakaokaidi amri hiyo watafikishwa mahakamani. 


Hadi sasa watu 15 wanaoshikiliwa na jeshi la polisi mara baada ya watu hao kukaidi amri ya kuondoka katika bonde la mto Msimbazi katika zoezi ambalo limefanyika kati ya tarehe 15 marc hadi tarehe 17 March.





 

0 comments:

Post a Comment