Mkurugenzi wa TPSF Mr. Louis na Mkurugenzi wa Kinyyago Travel Diana Gasper
Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF) kama mwamvuli wa taasisi binafsi nchini inaendelea kupongeza jitihada za serikali katika kuleta mabadiliko ya uchumi nchini, taasisi kwa kushirikiana na Kinyago Tours inandaa mipango ya biashara ya kwenda nchini china. lengo la ziara hiyo ni kuangalia mabadiliko ya kiviwanda katika adhma ya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Hii ni katika muendelezo ya mahusiano katika uwekezaji ukilenga kuondoa changamoto za kiufundi na kujifunza utaalamu ambayo nchi ya china inapitia katika maboresho ya viwanda na kufikia hapo ilipo kwa mrengo wa soko lake kiviwanda. pamoja na malengo mengine Tanzania itajifunza soko la usafirishaji la china na kulielewa.
Mahusiano haya yatahusisha matukio matatu muhimu; biashara ndogo na za kati kuanzia tarehe kumi hadi kumi na tatu aprili huko Shanghai, itafuatiwa onyesho la kimataifa la biashara la Canton huko Guanzhou kati ya tarehe 15-19 aprili, na hatimaye mkutano wa biashara kati ya Tanzania na china huko Guanzhou.
Katika ziara hiyo ya mahusiano wafanyabiashara watakao shiriki watapata fursa ya kutembelea viwanda maaruf, masoko pamoja na sehemu za kitalii.
Matukio haya ya ziara ya mahusiano yamegawanywa sehemu mbali mbali ili kumpa mshiriki fursa pana ya kuchagua.
Mkurugenzi wa Kinyyago Travel Diana Gasper







0 comments:
Post a Comment