Mashindano ya Kobil Kilimanjaro Rally yamekamilika
mkoani Moshi yamekamilika kwa dereva mkongwe Gerald miller kuwa mshindi wa mbio
hizo za magari zilizofanyika mkoani Kilimanjaro kwa siku mbili.
Gerald Miller alikuwa na msoma ramani wake Peter
Fox wakiwa na gari aina ya EVO IX na kufanikiwa kutumia muda wa saa 1:30:50.
Nafasi ya pili ilikwenda kwa Guroal Sandhu akisomewa
ramani na Sinder Sudle wakitumia gari aina ya EVO X na kutumia saa 1:42:51
nyuma ya Gerald Miller kwa dakika 9:01.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kobil Tanzania Bwn. Davis Mosha akikabidhi zawadi ya kikombe kwa Mshindi wa Pili wa Mashindano ya Kobil Kilimanjaro Rally 2017. |
Kwa upande wa nafasi ya tatu imekwenda kwa Dharam
Pandya na msaidizi wake Awadh Fadhil wakiendesha gari aina ya EVO IX na
kumaliza mbio hizo ndani ya saa 1:48:47 nyuma ya mshindi wa kwanza kwa dakika
14:57.
Katika zoezi la utoaji wa zawadi kwa washindi wa Kobil
Kilimanjaro Rally lililoongozwa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh Mecky Sadick
pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya Kobil Tanzania Davis Mosha.
Mkurugenzi wa Kobil Tanzania Bwn Davis Mosha akikata keki ya Klabu bora ya Mwaka ambayo imeshinda Kilimanjaro Motor Sport kwa Tanzania ambapo Davis Mosha ndiye Muanzilishi wa Klabu hiyo |
Mbali na washindi hao kupewa tuzo, kampuni ya
Africa Swahili Media ilipewa tuzo ya heshima kutokana na mchango wake mkubwa
katika mashindano hayo.
0 comments:
Post a Comment