Msanii Chinbees amewatoa hofu mashabiki zake kwamba hana ugomvi wowote na wasanii kutoka ‘Weusi’ pamoja na Producer Quick Rocka kutoka studio ya Switch na kwamba bado wanaishi kwa kusaidiana licha ya kuwa chini ya uongozi mpya kwa sasa.
Chinbees ambaye kwa sasa yuko chini ya menejimenti ya Wanene Entertainment, ameyasema hayo baada ya kuulizwa kama ana ugomvi na watu hao ambao wamemsaidia kunyanyuka katika ‘game’ ya bongo fleva mpaka kusainiwa katika ‘lebo’ inayoaminika kuwa na uwekezaji mkubwa Tanzania.
Chinbees
“Weusi pamoja na Quick Rocka wale ni kaka zangu, wananipatia misaada mingi tofauti hata na kazi za muziki, kwenye maisha ya kawaida wananisapoti sana kwa sababu wanajua mimi ni mdogo wao nahitaji nini, hata haya mafanikio madogo ambayo nimeanza kuyapata wanayafurahia sana”. Amesema Chinbees kwenye eNewz.
Kwa sasa Chinbees anatamba na ngoma inayokwenda kwa jina la Pepeta amesema kwamba yupo tayari kwa kolabo kubwa ambazo hata yeye mwenyewe zitamtoa kutoka sehemu moja kwenda nyingine, na kusisitiza kuwa hataki kufanya kazi ambazo hazimuongezei faida yoyote.
“Siyo kila project nitafanya, nitaangalia kama zina nafasi ya kunisogeza kwenda sehemu nyingine, yaani nazungumzia kazi kali ambayo hata nikishirikisha uongozi wangu hawawezi kukataa”. Alisema Chinbees
0 comments:
Post a Comment