MSANII
wa muziki wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Daimond Platnumz’, amempongeza
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa jitihada zake
kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa salama.
“Kwanza
kabisa Nimpongeze Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda kwa jitihada
zake. Ukizingatia ni mwaka mmoja tu tokea awe mkuu wa mkoa lakini
utendaji wake umezaa matunda mengi na changamoto ni nyingi zinazo
mkabili lakini bado amekuwa imara.”, alisema Diamond.
Diamond
ameyasema hayo leo katika mkutano kuhusu vita dhidi ya madawa ya
kulevya uliofanyika katika Bwalo la Polisi Oster Bay jijini Dar es
Salaam ambako Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, na viongozi wengine wa
serikali na taasisi mbalimbali walihudhuria.
CHANZO:UDAKU SPECIAL

0 comments:
Post a Comment