Wednesday, March 1, 2017


Timu ya McLaren imejikuta katika wakati mgumu kwenye michuano ya majaribio kabla ya kuanza kwa michuano mbalimbali katika mbio za langalanga licha ya mabadiliko kadhaa yaliyofanywa na Honda ili kuboresha injini za timu hiyo.


Vandoorne samesema yeye pamoja na dereva mwenzake wangefurahi zaidi kama wangeweza kumaliza mizunguko yote wakati wa mazoezi, hivyo kwa sasa anadhani ni jambo la busara kwa timu yake kuangalia namna itakavyoweza kukabiliana na changamoto zilizojitokeza ili zisijirudie.

Katika majaribio hayo, mbelgiji Stoffel Vandoorne alifanikiwa kumaliza mizunguko 40 tu akiwa amemzidi dereva mwenzake Fernando Alonso kwa mizunguko 11.
Gari ambalo alikuwa akitumia dereva Alonso lilipata matatizo kutokana na mfumo wa tanki la mafuta kushindwa kufanya kazi vema.
Fernando Alonso (kushoto) akiwa na dereva mwezake Stoffel Vandoorne (kulia) 


Honda imetambulisha injini mpya zenye mfumo wa turbo toka mwaka 2014 wakiwa wamefata falsafa ya timu ya Mercedes.

Siku ya Meneja anaehusika na maswala ya utengenezaji wa injini toka katika timu ya Honda, Yusuke Hasegawa alisema kwamba mabadiliko ambayo waliyafanya katika gari lao jipya yangeweza kuleta ushindani mkubwa lakini sasa imeonekana kuwa kuna baadhi ya kasoro.


Hata hivyo teknolojia iliyohusika taika utengenezaji huo imeleta mkanganyiko ndani ya Honda kutokana na timu hiyo kuifanya teknolojia hiyo ifanye kazi ipasavyo ndani ya gari la McLaren Honda.

0 comments:

Post a Comment