Mchezaji
nambari tatu kwa ubora katika mchezo wa gofu duniani Rory McIlroy amerudidhwa
nyuma sana na ukosoaji uliofanya na mashabiki wa mchezo huo pale aipocheza
mchezo huo na rais wa Marekani Donald Trump.
Rory, ambae sasa amerejea katika
michezo ya PGA inayoendelea nchini Mexico amesema mara baada ya kucheza na
bwana Trump ameonekana kuwa ni mtu mwenye kutumia mabavu pamoja na ubaguzi wa
hali ya juu.
Akizungumzia mazungumzo
yaliyokuwa yakiendelea wakati wakicheza gofu, Rory amesema mazungumzo yao
yalijikita katika mchezo wa gofu na hakuna jambo lolote lile la kisiasa
walilolijadili.
Licha ya kuwa na kuwa na umri wa
miaka 41, Rory bado anashiriki katika mashindano ya mabingwa yaani Masters – na
amefanikiwa kushinda mara nne.
Alipoulizwa na wanahabari kuhusu
mchezo wake dhidi ya Bwana Trump, Rory amesema alitekeleza agizo hilo kama
sehemu ya heshima kwani ingekuwa si rahisi hata kidogo kumkatalia rais kucheza
nae gofu.
Amesema hakubaliani nae kwa kila
analolifanya katika utawala wake japo yeye si mmarekani na wala hawezi kupiga
kura katika chaguzi mbalimbali za Marekani.
Katika hatua nyingine Rory amesema
amepata nafasi ya kuonana na aliyekuwa bingwa wa dunia katika mchezo huo
mkongwe Tiger Woods, na kusema kwamba hali yake kiafya imeimarika.
Tiger Woods amekuwa akisumbuliwa
na majeraha ya mara kwa mara katika mika aya hivi karibuni na hajarejea tena
viwanjani toka alipojitoa katika mashindano ya jangwani ya Dubai Desert Classic
mwezi February.

0 comments:
Post a Comment