Monday, April 3, 2017



Mbunge wa CHADEMA aliyekuwa amefungwa anadai gerezani wafungwa wanapoitia mateso makali na ametaja aliyoyapitia kipindi cha miezi 3 aliyokuwepo huko,
anadai kuwa kuna madawa ya kulevya yanauzwa jela kwa kiwango kikubwa na wanaouza wanafahamika waziwazi ila mkuu wa gereza anadai hajui.
Anadai alishawekewa bunduki kichwani na askari akimuambia akachukue kuni na askari akimfuatilia na bunduki nyuma. Amesema pia alikuwa akiumwa Malaria na daktari akamuambia apumzike ila askari akamlazimisha akabebe zege.

Licha ya kupitia mateso hayo lakini amedai hatakuwa mpole, ataendelea kupambana tu akiona amezinguliwa amedai pia kuna mfungwa aliyekuwa ameongea na DW kuhusu mateso ya gerezani lakini alipigwa vibaya sana na askari.

0 comments:

Post a Comment