
Msanii maarufu wa Bongo Muvi JB wikiendi hii amezua mtafaruku mzito baina ya Wasanii baada ya kualikwa Ikulu kuhudhuria Chakula cha Usiku kwa ajili ya Waziri Mkuu wa Ethiopia,
aliyekuwa hapa nchini kwa ziara ya Siku mbili. Mtafaruku huo ulizuka pale tu JB alipotundika picha ya kwanza akiwa Ikulu kwenye dhifa hiyo, Wasanii mbali mbali wakubwa nchini walizana kuulizana kwamba nani kamulika JB huko na kwa msingi gani huku kuna Viongozi wa Chama cha Wasanii ambao ndio hasa waliopaswa kualikwa walidai Wasanii hao. Kurasa mbali mbali za Wasanii maarufu nchini huko Instagram zilianza kuhoji mualiko huo kwa maneno mengi ya mafumbo mafumbo, pitia kurasa za Wasanii hao wa Bongo Muvi huko Isntagram ujionee mwenyewe.
0 comments:
Post a Comment