Wednesday, May 3, 2017

Mkongwe wa hip hop na Mfalme wa mashahiri kutokea mji kasoro bahari Afande sele amefunguka na kudai wasanii wa sasa wana roho mbaya na kukosa upendo hali inayo wapelekea kuharibiana hadi nyimbo.

Afande Sele amefunguka hayo hivi karibuni na kusema kuwa wasanii wa sasa wengi wao wanafanya uimbaji kama mashindano kwa sababu kila mmoja anataka kuonekana mkali zaidi ya mwenzake.
"Wasanii wa sasa hawana upendo kabisa, roho mbaya kila mtu anataka kuonekana ni mkali kuliko mwenzake. Sisi tulikuwa na upendo mwenzetu akiwa na show wote tulikuwa tunakutana na kupanga mikakati show itajaza vipi lakini sasa hivi ni kama vita yale mapenzi na upendo tuliokuwa nao vijana wa sasa ndiyo wamenyimwa"- Afande Sele.
Aidha afande aliendelea kufunguka " Mimi nilimsifia msanii Darasa kuwa ndio msanii bora wa Hip hop kwa sababu alitoa wimbo ukawa kama wa taifa wakaibuka watu wengine ambao wanafanya muziki usioeleweka, wengine kama huyo huyo Darassa wakasema kwamba Darassa hafanyi Hip hop. Sasa kwani mafanikio ya Darassa si ndio mafanikio ya Hip hop lakini hawataki hizi ni chuki kabisa"- Afande alizidi kufunguka.
Afande ameenda mbele zaidi na kufunguka kwamba imefikia sehemu wasanii wanadiriki kuharibiana nyimbo wanazoshirikiana na kutolea mfano msanii Baghdad alivyokata tamaa katika kufanya poa kwenye nyimbo za wenzake tofauti na ilivyokuwa awali.
"Baghdad ni mzuri sana laki akitoa wimbo aliofanya mwenyewe haupokelewi na akitoa ameshirikiana na mtu watu wanabadilisha ngoma na kuhisi yeye ndiyo kashirikishwa sasa hivi anaimba ili mradi tuu na yeye akishirikishwa, ile morali ya zamani imekata kabisa"- Afande Sele.

0 comments:

Post a Comment