Thursday, May 4, 2017

Msanii Afande Sele ambaye ametokwa na povu baada ya Rapa Wakazi kutaja list ya wasanii akiwepo Fid Q, Zaiid, P The MC kuwa ndiyo wafalme wa rhymes kwa bongo huku akimtoa Afande Sele na kusema Afande yeye ni mkali ila siyo kiufundi 'technically

Baada ya kauli hiyo ya Wakazi ndipo alipoibuka Afande Sele na kusema yeye hamjui wala kumfahamu mtu anaitwa Wakazi hivyo Rapa huyo anatafuta kiki kupitia mgongo wake.
"Wakazi ndio nani hata kwa sura simjui. Sijwahi kusikia kazi yake hata moja, au ndio kiki za kutaka mtoko? Chocolate rapa", alisisitiza Afande Sele 
Kufuatia kauli hii ya akaibuka Wakazi na kusema Afande Sele amekasirika baada ya kupewa ukweli kwani kiufundi kweli hawezi kuwazidi wasanii hao aliowataja na kusema yeye hajali kama anasema hamjui.
"Kama wewe hunijui sio kesi, ila wakuitwaga Rakim 'The God Emcee knows me' Unless useme you are better than him too technically..Aliyeimba kuhusu "Mtazamo" kusanifu uwezo wa wasanii wenzake, leo anakasirika wasanii wenzake kutoa mtazamo wa uwezo wake" alisema Wakazi 

0 comments:

Post a Comment