Tangu wagome kuandika Habari zako, na kukutangaza kwenye TV na radio wanazomiliki nimemuona Mungu akiendelea kukutangaza kwa jamii kupitia watu aliokutaarishia, tunasoma habari na kuona kazi unazofanya kupitia mitandao ya kijamii mfano magroup ya what's app, facebook, instagram, twitter .Leo nataka kusema jambo moja kubwa ambalo limegusa MOYO wangu na wa familia yangu nalo si lingine bali NI "MAONO YAKO YA KUWAONDOLEA KERO KINA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WA MKOA WA DSM."

Nimeona picha ya Ujenzi wa majengo ya kisasa ya wodi za kina mama na watoto katika Manispaa tatu za Mkoa wako yaani, Ilala pale Amana, Temeke pale Temeke Hispitali na Kinondoni pale Hospitali ya Mwananyamala yenye ghorofa tatu kila moja na uwezo wa kulaza kina mama na watoto wao 450 kwa wakati mmoja, hakika hili lilikuwa ONO kutoka kwa Mungu kupitia wewe.
Nasema haya ni MAONO yako kwa sababu umekuwa mkuu wa Mkoa wa kwanza Tanzania tangu tupate uhuru ambae ulibuni wazo hili la kujenga hizi Wodi pasipo kutumia FEDHA yoyote kutoka Serikalini, zaidi ya akili, busara na mawazo yako ya kuwahamasisha wawekezaji kukuunga mkono katika MAONO haya ambayo sasa YAMETIMIA.
Najua waandishi wa Habari hawatathubutu kusema haya au kuyatangaza haya, lakini sisi WANANCHI ambao unatusaidia usiku kucha TUTASEMA tu.

Niwakumbushe waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vilivyogoma kuandika Habari zako kuwa UNGEWEZA maono haya ukayatumia kwa FAIDA yako kwa kuwaomba wakujengee wewe JUMBA ZURI LA KIFAHARI LA KUISHI, lakini ulitutanguliza sisi wananchi mbele katika MAONO yako.
Ungeweza pia kutumia fursa hii kutajirisha ndugu zako na marafiki zako ambao LUKUKI ambao walikuwa wamekuzunguka kwa lengo la kukutumia wewe ili WAJINUFAISHE ZAIDI WAO, ila tunashukuru ulisimama imara na kutanguliza maslahi ya taifa mbele na haswa sisi wananchi wa kipato cha chini na leo TUNANUFAIKA SISI uku tukishuhudia "WALIOKUWA" marafiki zako wa "KIMASLAHI" wakikugeuka na kuungana na makundi yanayopambana na wewe, sisi WANANCHI TUNAJUA, NA TUNAWAJUA WOTE.
Nimalize kwa kuwakumbusha hao waandishi na wamiliki wa vyombo vya Habari waliogoma kuandika habari zako hata hizi zenye maslahi kwa familia zao kuwa, IKO SIKU HIVI VITANDA watakuja kulala wake zao na watoto zao japo wamegoma kukutangaza.
Wanasusa kuandika HABARI zenye maslahi na familia zao haswa wake zao na watoto zao ambao ni wanufaika wakubwa wa haya MAONO yako, IKO SIKU WATAKUJA KUSUTWA NA NAFSI ZAO NA HIYO SIKU HAIKO MBALI.
MAKONDA endelea kumwabudu na kumtumikia Mungu pasipo KINYONGO sisi wananchi tunaona unachokifanya na Mungu atakutangaza popote pale DUNIANI.
Ni mimi mwananchi wa Dar es salaam
MDASHIRU HAMAD SULEIMAN.

0 comments:
Post a Comment