
May 13, 2017 kulizagaa taarifa ambazo zilikuwa zinadai kuwa mmoja wa wadau wakubwa wa Simba SC Mohammed Dewji ‘MO’ anataka alipwe kiasi cha Tsh. 1.4b kutokana na klau hiyo kukiuka makubaliano ya kuingia mkataba wa udhamini na SportPesa.
Klabu ya Simba kupitia kwa Makamu wake wa Rais imetoa tamko:
“Uongozi utatoa tamko katika muda muafaka juu ya suala hili la Muingiliano wa Mkataba wa Sportpesa na uwepo wa MO ndani ya Simba SC.
“Mengi yanaongewa tena kwa upotoshwaji uliopitiliza. Tuna mechi mbili mbele yetu ambazo ni muhimu zaidi kwa sasa. Tunaomba utulivu na uvumilivu wenu.”
Natanguliza Shukrani.
Geofrey Nyange,
Makamu wa Rais.

0 comments:
Post a Comment