Mkuu wa mkoa leo amefanya kikao cha kazi na wakuu wa wilaya, wakurugenzi,wenyeviti na wajumbe wa MABARAZA ya ardhi wilaya, kata za jiji la mbeya, wanasheria wa halmashauri na maafisa ardhi Awataka wakurugenzi wa halmashauri zote kuwawezesha wanasheria wa halmashauri na maafisa Ardhi kutoa mafunzo kwa MABARAZA YA Ardhi YA vijiji na Kata ili kuelewa majukumu yao
Baadhi YA wenyeviti na wajumbe wa mabaraza haya ngazi za Vijiji na Kata hawana uelewa wa majukumu yao
Asema utaratibu aliouweka wa kusikiliza kero kati YA wananchi 500 aliowasikiliza 39 kati yao wamelalamikia utendaji wa MABARAZA ya Ardhi Malalamiko aliyoyapokea wamelalamikiamabaraza YA Ardhi kwa kutoza Ada kubwa , Rushwa, uchekeweshaji wa kesi na lugha chafu

- Amewataka wenyeviti na wajumbe kuanzia leo na mara baada YA mafunzo watakayoyapata kuanzia wiki ijayo wabadilike na kurejesha imani kwa wananchi
- Amekiri pia mabaraza hayo yanachangamoto za majengo, uhaba wa watumishi, vitendea kazi na hivyo kuwataka wakurugenzi kutenga bajeti kuboresha utendaji kazi wa mabaraza hayo

0 comments:
Post a Comment