Mmiliki wa shule ya Lucky Vincent ambaye anatambulika kwa majina ya Innocent Mushi amefikishwa kartini leo jijini Arusha na kusomewa mashataka manne kuhusu ajali ya gari lake ambalo lilikuwa limewabeba wanafunzi siku ya ajali.
Gari hilo aina ya ‘coaster’ lilisababisha vifo vya watu 35 baada ya kutumbukia katika korongo na kukatisha uhai wa wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent Nursery & Primary School 32, walimu wawili wa shule hiyo pamoja na dereva ambaye alikuwa akiendesha gari hiyo.

0 comments:
Post a Comment