Mwanamuziki Witnes 'Kibonge Mwepesi' amemtetea 'producer' Master J kuhusu uvumi wa kuhusika katika kuliua kundi la 'Wakilisha lililokuwa na wasanii watatu ambao ni Langa, Shaa pamoja na yeye mwenyewe na kudai aliyekuwa meneja wao ndio chanzo.
Witness amefunguka hayo hivi karibuni alipokuwa kwenye heshima ya bongo fleva ya Planet Bongo na kusema siyo kweli kama tetesi za mitaani zinavyodai (Master J) alikuwa akiwadhulumu kwani 'Producer' huyu hakuwahi kuhuisika kwa namna yoyote kwenye kundi bali alikuwa kama mshauri wakati mwingine.
"Mater J hakuwahi kuwa Meneja wa kundi la Wakilisha bali yeye alikuwa kama producer mwakilishi kutoka nchi ya Tanzania. Kuvunjika kwa kundi la Wakilisha kulichangiwa na uongo uliokuwa unaendekezwa na Meneja Dan ambaye alikuwa akitufanyisha kazi nyingu Mapato kidogo"- Witness alifafanua.
Aidha aliendelea kufunguka "Waandaji wa Mashindano kumbe walikuwa wakitoa pesa kama mishahara ili tuweze kujikimu kimaisha lakini hata zile zilikuwa zinapita tusipopajua siku hiyo ndo tunafunguliwa macho tunaulizwa si mnalipwa Million tano ikabidi tushangae kwa sababu tulikuwa tukifanya Show tunalipwa laki tatau tu"- Witness aliendelea kufunguka.
Pamoja na hayo Witness ameeleza kuwa walishindwa kumshtaki meneja wao kwa waandaji wa Coca Cola Pop star kwa sababu tayari siri na mipango waliyokuwa wamepanga ilivuja na kumfikia Dan.
0 comments:
Post a Comment