Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS ), Tundu Lissu amewataka wafanyakazi wa Shirikisho jipya la Wafanyakazi nchini (Taffetu) kuungana pamoja na kujitambua ili waweze kutetea haki zao.
Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) alitoa kauli hiyo kwenye maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi jana zilizoandaliwa na shirikisho hilo ambayo kitaifa yamefanyika mjini Dodoma ambapo amesema kuwa licha ya kuwa shirikisho hilo linawafanyakazi wachache isiwe kisingizio cha wao kutofanya maamuzi ya pamoja.
Mhe. Lissu ameongeza kuwa wao kama wafanyakazi, wanapaswa kuwa na umoja wenye nguvu, pia wanapaswa kujitambua ndipo watakuwa na nguvu kubwa ya kudai haki zao za msingi.
Hata hivyo Tundu Lissu hakusita kuvizungumzia vyama vya wafanyakazi vilivyounda TUCTA akisema kuwa vingine vinajisahau kuwa kazi yao ni kutetea maslahi ya wafanyakazi.
0 comments:
Post a Comment