Wednesday, May 3, 2017

Idris Sultan amefunguka sababu ya kukosa nafasi ya kua host katika tuzo za MTV MAMA mwaka jana japo alionekana kupata kura nyingi katika kinyang’anyiro kile.

Idris alikuwa anashindana na mastaa wengine wakubwa duniani wakiwemo Basket Mouth (Nigeria), Idris Elba (Uingereza) na Kevin Hart (Marekani).
“Nilikuwa natakiwa niwe host lakini sasa sijulikani duniani, kwa sababu MTV MAMA inaangaliwa duniani kote. Host anatakiwa ajulikane angalau kidogo duniani. Ikawa ngumu sana mimi kupewa kuhost ingawaje nilishinda kwenye zile nomination, kwa hiyo ilibidi nihustle chini kwa chini ili na mimi nifanye kitu. Niligomba lakini niliwaambia jamani nitakuja hata bure hata ndege nitajilipia. Nakumbuka ndege nilijilipia, lakini hotel ndio hivyo sawa mpaka nikafika pale,” amekiambia kipindi cha The Playlist cha Times FM.
Nafasi ya Idris kuhost katika tuzo hizo lichukuliwa na Trevor Noah lakini siku chache kabla ya kufanyika tuzo hizo aliahirisha na nafasi hiyo ikachukuliwa na Bonang Matheba pamoja na Yemi Alade.

0 comments:

Post a Comment