Posted by Williammalecela.com on Friday, June 09, 2017
 |
Kutoka Bungeni Dodoma leo June 8, 2017 Waziri wa Fedha na
Mipango Dr. Phillip Mpango aliwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka
wa Fedha 2017/18, hivi ni baadhi ya vitu ambavyo wakati vinasomwa
viliwafanya wabunge wapige makofi kwa wingi na hata kusimama
wakishangilia.
1.Waziri ametangaza kufuta ada ya mwaka ya magari iliyokuwa
inalipwa hata kwa magari ambayo hayatumiki badala ada hiyo italipwa kwa
magari yanayotembea tu , Waziri amesema wamefuta ada hiyo ili ilipwe
mara moja gari linaposajiliwa baada ya hapo liendelee kulipiwa kwenye
ushuru wa bidhaa za petrol na diesel aidha Serikali imetoa msamaha wa
kodi, riba na adhabu zinazoambatana na madeni yote ya ada hiyo.
2.Kusamehe ongezeko la thamani
kwenye vyakula vya mifugo vinavyotengenezwa hapa nchini ili kupunguza
gharama za kununua vyakula hivyo kwa wafugaji.
3.Waziri amependekeza kutoza kodi ya ongezeko la thamani kwa
kiwango cha asilimia 0 katika huduma zinazotolewa kwenye usafirishaji wa
bidhaa na mizigo nje ya nchi ili kuifanya Tanzania iwe njia bora ya
kupitisha bidhaa zinazotoka nje ya nchi kwenda nchi zingine.
4.Kingine alichokisema Waziri
Mpango ni kuwa Serikali haitaruhusu usafirishaji wa madini kutoka
migodini na kupeleka moja kwa moja nje ya nchi aidha Serikali itaanzisha
maeneo maalum latika viwanja vya kimataifa, migodini, bandarini,
mipakani ambapo madini hayo yatathibitishwa na kupewa kibali cha
kusafirisha madini hayo ambacho kitatozwa ada ya 1% ya thamani ya madini
hayo.
5.Mtu anayesafirisha mazao yake kutoka halmashauri moja hadi nyingine yasiyozidi tani moja asitozwe ushuru
6.Kutoza ushuru wa forodha kwa
kiwango kwa asilimia 0 badala ya 25% kwenye malighafi na vifaa
vinavyoagizwa nje ya nchi kwa ajili ya kuunganisha na kutengeneza vifaa
ambavyo ni mahususi kwa ajili ya matumizi ya walemavu
7. Kufutwa kwa Ushuru wa mabango yanayoelekeza mahali huduma za jamii hususani shule, hospitali na zahanati zinapopatikana |
0 comments:
Post a Comment