Kwa jinsi mauaji yanavyofanyika mkoa wa Pwani nadhani ni ujumbe mzito kwa Serikali toka awamu ya nne.
Wauaji wanaua Polisi,Mgambo,viongozi w Serikali za mitaa na
viongozi wa CCM tu na hawagusi kabisa wake zao wala watoto wao wala
ndugu wa familia zao.
Kwa mtazamo wangu hapa Kuna kazi kubwa ya kufanya kujua root cause
lakini sidhani kabisa kama ni uhalifu kama nilivyoeleza ktk kichwa cha
mada. Wauaji wameamua kuchagua eneo la mkoa wa Pwani kutokana na
jiografia yake ilivyo ikiangalia Mkuranga,Kibiti na Ikwiriri ni rahisi
sana watu wenyewe nia mbaya kutua kimkakati kufanikisha nia yao.
Serikali Inahitaji intelejensia ya ziada kapata root cause.
IGP kutangaza 10 mil hakuna atakayeichukua kwasababu hakuna
atakayekubali kuuwawa kwa 10mil kutokana na wapewa siri kutotunza siri.
IGP tuko Pamoja ila Kuna kazi ya ziada fikiria Nje Pwani Kuna uwezekano ndiyo root cause.
Majeshi mengi yaliyopo Pwani hayatasaidia Kitu kwasababu wanapigana na invisible killers.

0 comments:
Post a Comment