Thursday, June 8, 2017


       Kweli duniani Kuna Mengi : Sintofahamu ya kifo cha Aliyekuwa Mume wa Zari yazidi kutanda baada ya taarifa kutoka vyombo vya usalama vya Afrika Kusini Kutoa ripoti yake.
Katika ripoti hiyo Polisi wamesema Ivan Aliingia Afrika Kusini Mwaka 1999 na aliishi katika mji wa Laudium, Central Pretoria na baadae kuhamia Sandton Johannesburg. Kwa muda wote aliokaa Afrika Kusini alikuwa akifanya Deals Chafu za kumuingizia pesa.

Kazi ya Kwanza Kufanya: Kazi ya kwanza kufanya Ivan baada ya kuingia Afrika kusini ilikuwa ni Uganga wa Kienyeji na alijipatia pesa kwa kujifanya kuwa ni Mganga anayewapa watu bahati na Mganga wa Mapenzi, Shughuli hiyo ilimpatia pesa nyingi na kuwaajiri vijana wa Kiganda Huko Afrika Kusini kama Ma agent wa Uganga wake, Kipindi hicho akiwa anatumia jina la “Shaba wa Shaba”. Jina Linalojulikana Afrika Kusini: Ivan Semwanga ni jina linalofahamika huku Africa Mashariki tu, Vyombo vya Dola Afrika Kusini vimefanya utafiti na hakuna record yoyote ya Ivan Semwanga na wamegundua kuwa Ivan alikuwa anafahamika kwa Jina la “Moreki Finder” jina ambalo lilikuwa linatumika hadi facebook kwa shughuli za Kiganga na kutapeli watu.

  Wameenda Mbele zaidi na kusema asilimia kubwa ya watu wametapeliwa na Ivan ambaye walimjua kama Mganga akitumia jina la Moreki Finder, hasa watu wa migodini aliwatapeli kwa kuwapa dawa za kupata Madini. Upekuzi Katika Chuo Chake: Vyombo vya Usalama pia vimefanya uchunguzi katika Chuo inachosemekana anakimiliki cha Brooklyn City College na kukutana na Haya, katika nyaraka zote za Chuo hakuna jina Ivan Semwanga na kwenye List ya wamiliki kuna Jina la Zari Hassan kama mmoja wa wamiliki pamoja na MS C Sullivan na R. Nsimbe.

Chombo kimoja cha habri Afrika Kusini pia kimeripoti kuwa Ivan Alikuwa yuko karibu sana na Mganga mmoja wa kienyeji Afrika Kusini Ajulikanaye kama Zamokwakhe “Bhaka”Nzamo na wamekuwa wakishirikiana mara nyingi kupiga deals chafu kwa pamoja. Katika Idara ya Uhamiaji: E! Pepa tumepata taarifa ya Idara ya Uhamiaji nchini Afrika Kusini kuwa katika list ya watu waliokuwa wakiishi nchini Afrika Kusini ambao ni raia wa Uganda Kuna Jina Ivan Ssemwanga na Jina lingine la Ali Sennyomo ambalo ndio alikuwa akilitumia Mara nyingi anaposafiri, Passport hizi mbili alizitumia kwa nyakati tofauti kulingana na mchongo anaokwenda kupiga. Mpaka Sasa Vyombo vya Usalama vina Mashaka kuhusu Kifo chake na Kuna Uchunguzi Unaendelea, Ukikamilika tutawaletea hapa hapa

0 comments:

Post a Comment