Thursday, June 8, 2017

HABARI za Uhakika tulizopokea kutoka Kwenye Source ya kuaminika ndani ya familia ya Ivan ni kwamba kikao cha familia kilikaa jana na kufanya maamuzi ya Mgawanyo wa mali za Ivan,
Kikao hicho kilichohudhuriwa na Rafiki wa Familia ambaye ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Kwagalana Group Geofrey Kirumira pamoja na Joseph Bbosa ambao ni marafiki wa karibu wa familia.

Kwa sauti moja kama ndugu walikubaliana kusimamia mali za Ivan mpaka pale watoto watakapokuwa wakubwa na kuweza kuzimanage wenyewe. Kikao hicho kiliamua kuwa Zari Hassan, Ritah Ssemwanga (Dada), Lawrence Muyanja (a.k.a. King Lawrence) na George Ssemwanga Pinto (Kaka wa Ivan) ndio watasimamia mali hizo mpaka watoto watakapofikisha Miaka 18. Zari amepewa kusimamia shule za Ivan na Brooklyn City College chuo cha Ivan pamoja na nyumba mbili zilizopo Africa Kusini (Santon Pretoria).

0 comments:

Post a Comment