Friday, June 23, 2017

Aliyekuwa Miss Tanzania namba mbili  mwaka 2006 na mwanamitindo kwa sasa, Jokate Mwegelo ametoa msaada siku ya leo katika kituo cha watoto yatima na wajane  cha Ahbaabul Khairiya kilichopo Mwananyamala B.

Jokate ametoa msaada huo kama zawadi yake ya Sikukuu ya Eid El-Fitri inayotarajiwa kuwa siku ya jumatatu ijayo kwa mujibu wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA).
Mrembo huyo ametoa mchele kilo 250, unga kilo 250, mafuta ya kupikia , mbuzi wawili pamoja na nguo za watoto na wanawake.
Mkuu wa kituo hicho, Ahmed Shebe amemshukuru mrembo huyo aliyetajwa na jarida la Forbe Afrika mwaka huu kuwa maoja ya vijana walio chini ya miaka 30 yenye mafanikio kwa msaada huo alioutoa kituoni hapo.

0 comments:

Post a Comment