Sunday, June 11, 2017

Mkongwe wa muziki toka Nigeria 2face, ameamua kuchangia asilimia 60 ya mapato kwenye nyimbo zake ilikusaidia wakimbizi.

Msanii huyo ambaye ni mwenyekiti wa taasisi ya Tuface, ametangaza kusaidia wakimbizi kupitia Shirika la wakimbizi dunia (UNHCR).
Kauli ya kusaidia wakimbizi ameitoa siku ya jana(Alhamisi) alipotembelea UNHCR jijini Abuja, na kusema kuwa atachangia asilimia hizo kwa nyimbo zake mbili mpya anazotarajia kuzindua siku ya wakimbizi duniani Juni 20.
“Nyimbo hizo zitauzwa kwa njia ya mtandao na zitagharimu kiasi cha N50 sawa na tsh/=344.17 hadi N100 sawa na tsh/=688.34.”alisema 2face, nae mwakilisi wa UNHCR katika mji huo, Bi Bridgette Mukanga-Eno ameishukuru taasisi ya msanii huyo kwa kujitolea kusaidia wakimbizi.

0 comments:

Post a Comment