![]() |
Akizungumza na waandishi wa habari, Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alisema kuwa ili matatizo ya unyonyaji kwenye sekta hiyo yakabiliwe kikamilifu, Tanzania inapaswa kuandika katiba mpya. Alisema kuwa mapungufu katika mikataba na sheria ya madini yamekuwa yakilalamikiwa na wapinzani kwa miaka mingi ndani ya Bunge lakini maoni yao hayakukubalika.
Wapinzani wameshasema sana, wakasema mikataba hii iletwe tuitazame upya kwenye Bunge, lakini walikataliwa,” alisema akiwataja baadhi ya makada wa vyama vya upinzani kama Tundu Lissu, John Mnyika na Zitto Kabwe waliowahi kuwasilisha ombi hilo. “Walikataliwa kwa sababu siri yake, jambo hili haliko kwenye katiba. Ndio maana mimi nasema tiba yangu moja kubwa ni kuhakikisha tunapata katiba mpya. Katiba ambayo itazitangatia maslahi ya wananchi katika kugawanya rasilimali zake,” aliongeza.

0 comments:
Post a Comment