Uongozi wa juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) unatarajia
kuwa na press conference, siku ya Ijumaa, Agosti 18, 2017
itakayofanyika jijini Dar es Salaam.
Kupitia mkutano huo, uongozi wa juu wa chama unatarajiwa kuzungumza na umma wa Watanzania kuhusu masuala mbalimbali muhimu kuhusu mwenendo wa nchi, kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Kutokana na uzito na umuhimu wa mkutano huo, chama kinaomba kukutana na wahariri na waandishi wa habari waandamizi wa vyombo mbalimbali vya habari (vya kitaifa na kimataifa) hapa nchini, siku hiyo, kuanzia saa 5 asubuhi, katika ukumbi ambao tutawataarifu jioni ya leo au mapema kesho asubuhi, bila kukwaza maandalizi ya vyombo vya habari kuweza kufika mapema, ndani ya muda, kwa ajili ya coverage.
======
UPDATES;
Viongozi wa juu wa CHADEMA wataongea na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam,Ijumaa 18/8/2017.Muda mfupi ujao.
=> Naomba nizungumzie athari za Serikali kuvunja mikataba ya wawekezaji wa nje" - Tundu Lissu
=> Wanasheria wanaoishauri Serikali wamekuwa hawatekelezi wajibu wao inawezekana ni kwa sababu ya kuogopa kutumbuliwa - Lissu
=> Ndege iliyotarajiwa kuwasili mwezi uliopita mpaka sasa haijafika na Serikali ipo kimya
=> Ndege hiyo iliyotarajiwa kufika mwezi uliopita imekamatwa na inashikiliwa Canada na wadeni wetu
=> Baada ya Waziri wa mambo ya nje kwenda Canada, Kampuni hiyo imekubali kuiachia ndege hiyo kwa malipo ya awali
=> Kwanini hilo deni halikulipwa mpaka miaka saba baadae ambapo deni hilo limeongezeka
=> Msisitizo wa Waziri wa mambo ya nje kutaka jambo hili liwe kimyakimya ni kwa ajili ya kumlinda nani?
=> Waziri Mbarawa alimjibu Zitto kuhusu ndege hiyo lakini hakusema ni taratibu zipi ambazo zimechelewesha ndege hiyo kuletwa
=> Nasema si kwasababu napenda kuyasema, ni kwasababu nalazimika kuyasema.
=> Baada ya Waziri wa mambo ya nje kwenda Canada, Kampuni hiyo imekubali kuachia ndege hiyo kwa malipo ya awali.
=> Tunaiomba Serikali iweke hadharani kesi zote ambazo tumeshitakiwa kwenye kesi za usuluhishi nje ya nchi.
=> Yote ambayo tumeyasema tuna ushahidi wa nyaraka, tuna nyaraka za kuthibitisha kila tulichokisema.
=> Kuna watanzania Wazalendo waliomo ndani ya Serikali hiihii ambao wametupa hizi nyaraka
=> Mimi ni mwanasheria natakiwa nisitaje chanzo lakini mjue tuna nyaraka za kuthibitisha kila tulichokisema

0 comments:
Post a Comment