Mkuu wa mkoa amezindua mkakati wa kuboresha elimu ktk Mkoa wa mbeya sambamba na kuongeza ufaulu ktk Shule za msingi na sekondari
- Mkakati huo umehusisha maafisa elimu wa wilaya, wakuu wa Shule, wenyeviti wa bodi na waratibu elimu kata
Ameelekeza kila Mtendaji ktk sekta YA elimu awe na mpango kazi na kutekekeza na walimu wazingatie ratiba YA ufundishaji
- Amezitaka bodi za shule kuwa kiungo na wananchi, kuthibiti nidhamu mashuleni
- Waratibu Elimu na watendaji ngazi zote wahamasishe jamii kuboresha miundombinu YA shule ikiwemo madarasa, hostel, vyoo na nyumba za walimu na wazazi waone umuhimu wa wanafunzi kupata chakula shule
- wakurugenzi na maafisa elimu washughulikie madai YA walimu na kuweka vivutio kwa walimu ikiwemo motisha kwa watakaofaulisha vizuri




0 comments:
Post a Comment