Posted by Williammalecela.com on Friday, August 04, 2017
_*NEEMA SEKTA YA AFYA DAR ES SALAAM.*_ Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Mheshimiwa _Paul Makonda_ leo amepokea *Vitanda 150* na *Magodoro
150* vyenye tamani ya zaidi ya *shilingi Million 300* kutoka kampuni ya
mafuta ya *Camel Oil* iliyoamua kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa
katika kuboresha sekta ya Afya. Akizungumza baada ya kupokea
Vitanda hivyo, _Makonda_ amesema amedhamiria kuhakikisha changamoto zote
zinazoikabili sekta ya Afya katika Mkoa wa Dar es Salaam zinamalizika lengo likiwa ni kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora za afya.
_*“Sitaacha kutafuta kwa ajili ya Wananchi wa Dar es salaam, nitabisha
hodi kila panapostahili ilimradi Wananchi wangu wawe wanapata huduma za
Afya katika mazingira mazuri. Na siku moja waone kazi kubwa inayofanywa
na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr. John Magufuli. Sisi
tunataka Maendeleo na maendeleo hayana chama,dini wala kabila. Jukumu la
kuuendeleza Mji huu wa Dar es salaam ni jukumu letu sote kama wakazi na
wananchi wa mkoa huu”*_ Alisema Makonda. _Makonda_ amesema
anatamani siku moja kila mama anaekwenda kujifungua alale kitanda kimoja
mwenywe na sio kama ilivyo sasa ambapo wanatumia kitanda kimoja kina
mama watatu hadi wanne.
0 comments:
Post a Comment