Msanii wa Bongo Flava, Lulu Diva amesema hajawahi kuwa danga kwani chochote kinachoonekana kwenye maisha yake anakimiliki yeye.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Give It To Me’, kuwa licha ya kutokuwa na danga yeye ni msichana wa gharama na asiyefeki maisha kama baadhi ya watu wanavyodhani.
“Sijawahi kuwa danga kiukweli kwa sababu sioni umuhimu wa kuwa na danga and that why nimewachana katika ngoma yangu ya Utamu. Hao wanaongea kuwa nafeki maisha hadi maji wanakopa mimi sichukulii ni big dili, kwa hiyo sio kitu kibaya one day watakubali kuwa Lulu hivi ndivyo anaishi,” amesema na kuongeza.
“Lulu ni msichana ambaye ni very expesive, ni msichana ambaye anaisha maisha very expensive kuliko hata huyo ambaye anaongea, actually napenda maisha mazuri ndio jinsi mimi nilivyo and mimi siishi maisha feki chochote ambacho unaona niponacho ujue ni cha kwangu,” amesema.
0 comments:
Post a Comment